Sunday, January 20, 2013

Historia kifo cha Dr Kleruu

 Mwanzoni mwa miaka ya 1970 Mwamwindi alikabiliwa na shitaka la kumwua Dr Wilbert Kleruu, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa wakati huo.
Mnara wa Kumbukumbu ya sehemu alipouwawa Dr Kleruu
Mshitakiwa Mwamwindi alijitetea kuwa alipokuwa anamwua marehemu Kleruu alirukwa na akili akapotewa na fahamu ya kuweza kuelewa kile alichokuwa anakitenda. Jaji Onyiuke alikataa hoja hiyo kwa kutilia maanani kwamba baada ya mshitakiwa kughadhibishwa ndipo alipokwenda ndani kuchukua bunduki ambayo aliitumia kumwua marehemu.  Inasimuliwa, kuwa ilikuwa siku ya Jumapili tar 25 desemba pale Mkuu wa Mkoa, Dr Kleruu, alipofika Isimani na kumkemea Mwamwindi mbele ya wake zake kwa vile alifanya kazi za shamba siku ya Jumapili.

Inasimuliwa, kuwa Dr. Wilbert Kleruu alifikia hata hatua ya kuanza kudhihaki makaburi ya mababu zake Mwamwindi akimwambia Mwamwindi: “Humu ndimo mlimozika mirija yenu”. Mwamwindi alikasirika sana. Akaficha hasira yake kutoka makaburini wakaongozana na Kleruu hadi nje ya nyumba yake. Akamwomba kiongozi huyo abaki nje, yeye akaingia ndani.

Mke wake Mwamwindi alimwona mume wake akichukua bunduki na kusimama dirishani. Mama huyo alidhani mume wake anakwenda kuwinda nguruwe. Kumbe, Mwamwindi alitokea dirishani. Mwamwindi akamlenga sawa kichwani Mkuu wa Mkoa na kumpiga risasi. Kisha akabeba mwili wa Mkuu wa Mkoa na kuuweka nyuma ya boneti ya gari alilojia mkuu huyo wa mkoa. Mwamwindi akaendesha gari hilo hadi kituo cha polisi Iringa. Akaripoti kwa kutamka; " Nendeni mkamchukue mbwa wenu nyuma ya gari!".

Tukio lile bado linatuachia maswali? Je, ni kwanini Dr Kleruu alikwenda nyumbani kwa Mwamwindi siku ya Jumapili?

Je, yawezekana Mwamwindi na Dr Kleruu walikuwa na ugomvi mwingine kabla ya tukio?





No comments:

Post a Comment